1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Umri wa kustaafu miaka 67

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKc

Bunge la Ujerumani Bundestag limeidhinisha kuongeza umri wa kustaafu kutoka ule wa hivi sasa wa miaka 65 hadi kuwa miaka 67.

Hatua hiyo imepitishwa kwa urahisi kwa kura 408 dhidi ya 169.

Chini ya sheria hiyo mpya umri huo wa kustaafu utakuwa ukiongezwa kwa awamu kuanzia mwaka 2012 ili kuweza kufikia umri huo wa kustaafu wa miaka 67 ifikapo mwaka 2029.