1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Uvutaji kuzuiliwa maeneo ya umma

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByB

Bunge la Ujerumani-Bundestag-limeidhinisha mswada wa kupiga marufuku kuvuta sigara katika vyombo vya usafiri vya umma na kwenye majengo ya umma kuanzia mwezi wa Septemba.Mswada huo lakini kabla ya kuweza kuwa sheria,unahitaji kuidhinishwa na Bundesrat,ambalo ni baraza linalowakilisha mabunge ya mikoa 16 ya Ujerumani.Mswada huo pia umepandisha umri wa kuruhusu vijana kuuziwa sigara,tumbaku na kadhalika ,kutoka miaka 16 hadi miaka 18.Wizara ya afya ya Ujerumani inatathmini kuwa uvutaji sigara kila mwaka unaua watu 40,000 kwa njia moja au nyingine.Katika nchi za Umoja wa Ulaya,kila mwaka watu 650,000 hufariki kwa sababu ya kuvuta sigara na hugharimu idara za kuhudumia afya,Euro bilioni 130.