1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Vyombo vya habari vyachunguzwa

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcO

Zaidi ya waandishi wa habari 12 wa Ujerumani wako chini ya uchunguzi baada ya vyombo vya habari kuchapisha nyaraka za siri kuhusiana na juhudi za kupiga vita ugaidi.

Shirika la utangazaji la taifa ARD limesema nyaraka hizo zimetoka kwa kamati za bunge ambapo wajumbe wa kamati hizo nao pia wanachunguzwa.Waandishi wote wanaohusika inadaiwa kuwa wamezipata nyaraka hizo kinyume na sheria.

Uchunguzi huo umeshutumiwa na waandisi habari kadhaa wanasiasa na vyama vya waandishi wa habari.Baadhi wameuelezea uchunguzi huo kuwa sawa na shambulio kwa uhuru wa vyombo vya habari wakati wengine wamelielezea kuwa ni jaribio la kuwatisha waandishi.