1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wafanyakazi wa simu wagoma.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3I

Nchini Ujerumani kiasi cha wafanyakazi 10,000 wa shirika la simu la Ujerumani Deutsche Telekom wanafanya mgomo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi cha Ver.di kuhusiana na mpango wa kampuni hiyo wa kuhamishia nje ya kampuni hilo nafasi za kazi 50,000.

Msemaji wa chama hicho cha wafanyakazi Lothar Schröder amedai kuwa mpango huo wa kuzipeleka nafasi hizo nje ya kampuni hilo ufutwe.

Deutsche Telekom linapanga kutengeneza huduma mpya kwa wateja kwa ajili ya wafanyakazi 50,000 ambao watafanyakazi kwa saa nyingi zaidi na malipo kidogo.