1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wahamiaji kupewa vibali vya kubakia na kufanya kazi

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrb

Serikali ya mseto katika bunge la Ujerumani, imefanya mageuzi makubwa kuhusu haki za wahamiaji.Kuambatana na mageuzi hayo,kiasi ya wahamiaji 100,000 waliostahmiliwa kwa muda tu, sasa watapewa vibali vya ajira na watapaswa kutafuta kazi hadi mwisho wa mwaka 2009 ili waweze kubakia nchini kwa muda usio na kikomo. Wakati huo huo serikali kuu na serikali za majimbo zimekubaliana kuwa na mkakati mmoja wa kuwajumuisha bora zaidi wahamiaji.Serikali za majimbo zimesema,kiini cha mkakati wa kuwajumuisha wahamiaji ni kuwahimiza watoto wa kigeni wa kila umri kujifunza Kijerumani.Majimbo yote yanaazimia kuwa na mpango mmoja wa elimu- kuanzia shule ya watoto wadogo hadi chuo kikuu. Ili kuweza kutimiza lengo la kuwafunza lugha watoto wa wahamiaji,serikali za majimbo zinatazamia kutoa mafunzo maalum kwa walimu wake katika miaka mitano ijayo.