1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wanajeshi wawili wa Ujerumani wasimamishwa kazi

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyj

Waziri wa ulinzi wa Ujerumai, FranzJosef Jung ametangaza kwamba wanajeshi wawili wa Ujerumani waliopiga picha na fuvu la kichwa cha mtu nchini Afghanistan wamesimamsihwa kazi.

Wanajeshi hao ni miongoni mwa wanajeshi sita walioonekana kwenye picha zilizochapishwa na gazeti la Bild juzi Jumatano, ambazo huenda zilipigwa mwaka wa 2003 karibu na mji mkuu wa Afghansitan, Kabul.

Mmoja wa wanajeshi hao amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya picha hizo na kuthibitisha zilipigwa karibu na mji wa Kabul mwaka wa 2003. Amesema tabia hiyo ya wanajeshi ilisabishwa na hofu waliyokuwanayo ya kusshambuliwa na waasi.

Haya yanafuatia hatua ya runinga ya RTL hapa Ujerumani kuonyesha picha mpya za wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na mafuvu ya vichwa vya binadamu nchini Afghanistan. Picha hizo mpya huenda zilipigwa mwaka wa 2004.

Mwanasiasa wa chama cha Kijani amesema amepokea taarifa ya picha zaidi zinazoonyesha visa kama hivyo au vibaya zaidi.

Akizungumzia juu ya picha mpya zilizotolewa, Reinhold Robbe anayehusika na maswala ya jeshi katika bunge la Ujerumani amesema,

´Kufuatia msimamo halisi wa uchunguzi, inaweza kuaminiwa kwamba picha hizi mpya zilizopatikana zinadhihirisha ukweli.´

Waongoza mashtaka mjini Potsdam sasa wanasema wanaume saba wanahusika katika kashfa hiyo na wala sio sita kama ilivyoripotiwa hapo awali.