1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wanaopinga utandawazi washutumu kupigwa marufuku maandamano.

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0s

Kundi linalopingana na utandawazi la Attac limeshutumu vikali kupigwa marufuku kwa maandamano katika eneo la mkutano mwezi ujao wa kundi la mataifa tajiri G8 nchini Ujerumani, na kusema kuwa hatua hiyo inachokoza mambo.

Wataarishaji wa maandamano wanasema kuwa upigaji marufuku huo unakwenda kinyume na haki za msingi.

Usalama kabla ya mkutano huo utakaofanyika katika muda wa wiki tatu zijazo tayari umeimarishwa, na polisi wanapanga kuweka eneo la kilometa mbili ambalo haliruhusiwi mtu kuingia bila ruhusa kuzunguka eneo la mkutano katika mji ulioko katika pwani ya kaskazini ya Ujerumani wa Heiligendamm.