1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wanasiasa wataka sheria kali zaidi kupambana na ugaidi

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBS7

Nchini Ujerumani,wanasiasa wanatoa mito kwa serikali kupitisha sheria kali zaidi,kupambana na ugaidi.Mito hiyo inafuatia kukamatwa kwa watuhumiwa ugaidi 3 nchini Ujerumani.Waziri wa masuala ya ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble amekariri pendekezo lake kuwa kuruhusiwe upelelezi wa mawasiliano yanayofanywa kwa njia ya kompyuta.Wito huo uliozusha mabishano,umeungwa mkono na chama cha SPD na Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani.

Washukiwa 3 waliokamatwa,wameshtakiwa kupanga njama za mashambulizi ya kigaidi na kuhusika na kundi la kigaidi.Wawili ni raia wa Ujerumani na mmoja ni Mturuki.Washukiwa wengine 7,wangali wakisakwa na polisi,ikiaminiwa kuwa walihusika na njama ya kutaka kushambulia vituo mbali mbali nchini Ujerumani.