1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Wavitaji sigara wabanwa zaidi hapa Ujerumani

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNp

Baraza la mawaziri la Ujerumani limekubali kupiga marufuku kuvuta sigara katika usafiri wa umma na katika majengo ya serekali ya shirikisho. Pia serekali imekubali kupiga marufuku kuuziwa sigara watu wenye umri wa chini ya miaka 18, hivyo kuzidisha umri huo kutoka miaka 16. Amri hiyo ambayo bado itahitaji kupewa kibali na bunge inapangwa ianze kufanya kazi Septemba Mosi mwaka huu. Hatua hizo mpya za kuzuwia uvutaji sigara, hata hivyo, sio kali kama zile zinazotekelezwa katika nchi nyingine za Ulaya.