1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Waziri ataka jeshi la Ujerumani litumwe Dafur

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpO

Msaidizi waziri wa uchumi nchini Ujerumani ametowa wito kwa jeshi la Ujerumani kupelekwa kwenye jimbo la vurugu la Dafur nchini Sudan iwapo Umoja wa Mataifa itaomba msaada wa Ujerumani.

Heidemarie Wieczorek-Zeul ameliambia gazeti la kila wiki la Bild am Sonntag kwamba Ujerumani isingeliweza kukataa ombi hilo iwapo Umoja wa Mataifa itaomba.Amesema mauaji ya kimbari yanatokea taratibu huko Dafur.

Hivi sasa Umoja wa Afrika una wanajeshi 7,000 huko Dafur lakini wameshindwa kuzuwiya umwagaji damu katika jimbo hilo la magharibi mwa Sudan.Umoja wa Mataifa umekuwa ukitaka kukadhibiwa shughuli hizo za kulinda amani lakini serikali ya Sudan haikuliafiki pendekezo hilo.

Tokea kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Dafur hapo mwaka 2003 inakadiriwa kwamba watu waliopoteza maisha yao huo Dafur wanafikia 200,000 na wengine zaidi ya milioni mbili na nusu wamepotezewa makaazi yao.