1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleeza Rice ashauriana na Kansela wa Ujerumani, Angela ´Merkel

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZn

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleezza Rice, amekutana na Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel ambapo alimuarifu kuhusu ziara yake ya hivi karibuni Mashariki ya Kati.

Bi Condoleezza Rice amekutana na Bibi Angela Merkel siku moja baada ya kushauriana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, ambapo mawaziri hao wawili walitangaza kwamba kundi la pande nne linaloshughulikia mzozo wa Mashariki ya Kati litakutana mwezi ujao mjini Washington.

Kundi hilo linajumuisha Umoja wa Mataifa, Marekani, Russia na Umoja wa Ulaya.

Mkutano huo unatarajiwa utasaidia kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israil na Wapalestina.

Bi Condoleezza Rice anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, mjini London.