1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleeza Rice ashauriana na mwenzake wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier.

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZs

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleezza Rice, pamoja na mwenzake wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, wamesema kundi la pande nne linaloshughulikia mzozo wa Mashariki ya Kati litakutana mwezi ujao.

Baada ya mashauriano mjini Berlin, Frank-Walter Steinmeier amesema mzozo wa Mashariki ya Kati kwa sasa hivi unapaswa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kundi hilo linajumuisha Umoja wa Mataifa, Marekani, Russia na Umoja wa Ulaya.

Mawaziri hao pia waliuzungumzia mradi wa Iran wa nishati ya kinyuklia.

Kuhusu mradi huo, Bi Condoleezza Rice alisema:

“Jambo la kuzingatiwa na jumuiya ya kimataifa sasa hivi ni tabia ya Iran kukiuka kila uchao azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium”

Bi Condoleezza Rice aliurejea msimamo wa Marekani kwamba haitawasiliana ana kwa ana na Iran hadi itakapoacha kurutubisha madini ya uranium.