1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wito wa Rais Abbas kuondosha vikwazo

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCP2

Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina ametoa wito kwa madola makuu kuondosha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya serikali ya Wapalestina.Baada ya kukutana na Kansela Angela Merekel wa Ujerumani,Abbas amesema vikwazo hivyo “si haki“ na ameyahimiza madola hayo kuondoa vikwazo viliopo.Merkel,amekaribisha mapatano yaliofikiwa kati ya chama cha Fatah cha Rais Abbas na chama cha Hamas chenye msimamo mkali,lakini amesisitiza masharti ya Umoja wa Ulaya kuwa serikali yo yote ile ya umoja itakayoundwa na Wapalestina,lazima itambue taifa la Israel.Vile vile amekariri wito kwa Wapalestina kumuachilia huru mwanajeshi wa Kiisraeli,Gilad Schalit alietekwa nyara.Abbas amefungamanisha suala hilo pamoja na madai ya kuitaka Israel iwaachilie huru wafungwa wa Kipalestina.