1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela Angela Merkel alaani kisa cha kupigwa Wahindi wanane

22 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWs

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amelaani vikali kisa cha kuandamwa na kupigwa wahindi wanane katika kijiji cha Mügln katika jimbo la Sachsen.

Kansela Merkel amehimiza kisa hicho kifafanuliwe kwa haraka amesema visa kama hivyo vinachafua hadhi ya Ujerumani katika nchi za nje.

Kisa hicho na juhudi za kupambana na siasa kali za mrengo wa kulia ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika warsha ya baraza la mawaziri wa serikali kuu ya muungano.

Katibu mkuu wa baraza la Wayahudi nchini Ujerumani Stepühan Kramer amesema kuwa wawakilisi wa kisiasa daima wamekuwa wakitowa hoja zile zile bila ya jambo lolote kubadilika katika mkakati huo wa kupambana na hisia za chuki dhidi ya wageni.

India imeitaka serikali ya Ujerumani ichukue hatua za kuwalinda raia wake wanaoishi nchini humu.

Wahindi wanane walishambuliwa na kundi la vijana wa Kijerumani wanaotuhumiwa kuwa mafashisti mamboleo.

Watatu kati yao waliumizwa vibaya na vijana hao wa Kijerumani.