1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela Merkel ataka kasi zaidi kushughulikia azimio jipya la ulaya

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFJ

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amewataka viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya kulifanyia kazi haraka azimio jipya litakalopelekea mafanikio ya katiba ya Umoja huo.

Kansela Merkel ametaka pia kuwepo kwa mpango wa makubaliano ya kisiasa ifikapo mwezi June mwaka huu.

Alikuwa akizungumza mjini Berlin hapo jana katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 toka kusainiwa kwa mkataba wa Roma uliyofungua njia ya kuundwa kwa Umoja wa Ulaya.

Azimio hilo linafungua njia ya matayarisho ya mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya ifikapo mwaka 2009.Poland na Jamuhuri ya Czech zimesema kuwa hazioni sababu za kuharakisha kuelekea mkataba huo mpya.