1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela Merkel na Rais Putin kujadilia makombora ya kujihami

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gb

Rais wa Urusi Vladimir Putin anapanga kufanya mazungumzo na Kansela Wa Ujerumani Bi Angela Merkel hapa Ujerumani mwishoni mwa wiki hii.Mazungumzo hayo yanalenga kujadilia mipango ya Marekani ya kuweka makombora ya kujihami katika eneo la Ulaya Mashariki aidha mustakabal wa jimbo la Kosovo.

Kulingana na Bunge la Kremlin la Urusi mazungumzo hayo ya siku mbili yatakayofanyika mjini Wiesbaden ni moja ya mikutano muhimu katika uhusiano kati yao na Ujerumani.Hatua hiyo inapangwa huku Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleeza Rice akijiandaa kwa mazungumzo hii leo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ili kujaribu kupoza moto hoja hiyo ya makombora ya kujihami.

Urusi inapinga vikali mipango hiyo ya Marekani ya kuweka makombora ya kujihami katika Jamhuri ya Czech na Poland kwani yatailenga.Marekani kwa upande wake inasisitiza kuwa inalenga kupambana na mataifa hasimu kama Iran na Korea Kaskazini.