1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mawaziri washindwa kukubaliana juu ya hatua za usalama

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBS1

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble na mawaziri wenzake wa serikali kuu na majimbo yote 16 nchini humu wameshindwa kukubaliana kwenye mkutano wao maalum wa usalama.

Mkuatano huo ulijadili juu ya katafuta njia za kupambana na ugaidi kufuatia kukamatwa watuhumiwa watatu wiki hii hapa nchini Ujerumani.

Waziri Schäuble amekariri pendekezo lake kwamba idara za usalama zipeleleze kompyuta za watu binafsi katika juhudi za kupambana na ugaidi.

Chama cha SPD kinachounda serikali na chama cha CDU/CSU kimepinga pendekezo hilo.

Wakati huo huo pendekezo la waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Bavaria bwana Beckstein kwamba Wajerumani waliosilimu wachunguzwe limelaumiwa.