1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Miaka 63 tangu kufa waliojaribu kumuua Hitler

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgr

Leo ni siku ya kumbukumbu ya maafisa wa kijeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi mnamo mwaka 1944.

Maafisa hao waliuwawa baaada ya jaribio la kutaka kumuua Adolf Hitler katika kambi yake huko Poland.

Kumbukumbu hiyo ambayo imeingia mwaka wake wa 63 itafanyika mjini Berlin katika makao makuu ambapo maafisa hao wanne waliompinga Adolf Hitler akiwemo kiongozi wao Claus Schenk von Stauffenberg waliuwawa saa kadhaa baada ya kiongozi huyo kurejeshwa hapa nchini Ujerumani.

Adolf Hitler alinusurika kifo baada ya Stauffenberg kutega bomu chini ya meza.

Philipp Freiherr von Boeselager ni afisa wa pekee aliye hai, alihusika na njama ya kumuua Hitler lakini alinusurika kuuwawa kwa kuwa alitoroka.

Maadhimisho ya leo yanakwenda sambamba na uzinduzi wa filamu mpya juu ya maisha ya Claus Schenk von Stauffenberg.