1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mkutano mkuu wa Umoja wa Ulaya wafanyika leo Brussels

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpu

Ujerumani ambayo ni rais wa sasa wa baraza la Umoja wa Ulaya imependekeza wazo la kuweka kando suala la katiba kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za umoja huo unaofanyika leo mjini Brussels.

Ujerumani imesema hayo katika mada iliyotawanywa kabla ya kuanza mkutano.

Kwenye mkutano wao leo viongozi wa Umoja wa Ulaya walitarajiwa kujadili mswada wa katiba mpya kwa ajili ya umoja wao .

Lakini Ujerumani imetahadharisha kuwa mazungumzo ya viongozi hao yanaweza kushindikana kutokana na msimamo wa Poland kupinga mabadiliko katika utaratibu wa kupiga kura. Poland imetishia kutumia kura ya veto kupinga mabadiliko hayo.