1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Msumbiji kupata msaada wa Ujerumani

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AX

Rais wa Ujerumani Horst Koehler anaahidi kuendelea kusaidia nchi ya Msumbiji baada ya kumkaribisha kwa mikono miwili Rais Armando Guebuza.

Msumbiji ni moja ya mataifa manne iliyo katika ratiba ya Ujerumani ya maendeleo ya kiuchumi na misaada kwa mujibu wa Rais Koehler.Msumbiji inakabiliwa na umasikini mkubwa hata baada ya uchumi kukua kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Kulingana na taarifa yake iliyotolewa mapema Rais Koehler anatoa wito kwa Wajerumani kuwekeza nchini Msumbiji.

Rais Guebuza anajiunga na marais wa Benin,Botswana na Nigeria kwa mkutano wa siku tatu kati ya Ujerumani na Bara la Afrika.Mkutano huo ulioanza hii leo unafanyika mjini Eltville.