1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Naibu kansela asema chama kipigwe marufuku

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt8

Naibu kansela wa Ujerumani bwana Franz Münterfering amezungumzia juu ya uwezekano wa kufanya uchunguzi mpya kuhusu kukipiga marufuku chama cha mlengo mkali wa kulia cha National Democratic cha hapa nchini.

Bwana Münterfering amesema ikiwa uwezekano wa kukipiga marufuku chama hicho utakuwapo atasimama msitari wa mbele kuunga mkono hatua hiyo.

Ametaka vijana wa kijerumani waelimishwe zaidi ili waweze kuepukana na itikadi za mlengo mkali wa kulia.