1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Pendekezo la Schäuble juu ya kukabiliana na magaidi lapingwa

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUb

Pendekezo la waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble la kutaka kuanzishwa kwa programu maalum ya mtandao wa Computa ya kuwachunguza washukiwa wa ugaidi limepingwa vikali na wanasiasa wa humu nchini.

Aliyekuwa waziri wa sheria kutoka chama cha FDP Sabine Leutheusser-Schnarrenberger amemshutumu bwana Schäuble akisema amevuka mipaka. Shutuma pia zimetolewa na wanachama wa Social Demokratic SPD, msemaji wa chama hicho Dieter Wiefesputz alisema mpango huo hauwezi kukubalika kabla haujachunguzwa na pia utabidi uwekwe wazi na kila mmoja auone na kuulewa.