1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Serikali ya Ujerumani yawatambua wanajeshi waliokuwa na fuvu huko Afghanistan.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzA

Serikali ya Ujerumani imesema kuwa imewatambua watuhumiwa sita walioonekana katika picha za gazeti zilizowaonyesha wanajeshi wakilichezea bufuru la kichwa la mwanaadamu huko Afghanistan.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz- Josef Jung amesema, wanne kati ya watu hao hawafanyi kazi tena katika jeshi la Ujerumani, wakati wawili waliobakia watakabiliwa na mashtaka.

Muendesha mashtaka mkuu wa Postdam, Wilfried LEHMNN amethibitisha kufunguliwa kesi ya makosa ya jinai dhidi ya wanajeshi wanaotuhumiwa kuchafua “amani ya wafu“ nchini Afghanistan.

Muendesha mashtaka mkuu Lehmann anasema.

“Tumeshatuma mashtaka dhidi ya usumbufu dhidi ya wafu. Tumeshagundua mmoja wapo wa watuhumiwa na uchunguzi unaendelea“.

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezieleza picha hizo zilizochapishwa kuwa zinatia kinyaa na kutoa amri ya kufanyika uchunguzi wa haraka wa tukio hilo.