1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujejrumani yaanza kutumia sheria mpya dhidi ya ugaidi

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMJ

Serikali ya Ujerumani kwa mara ya kwanza inatumia sheria mpya dhidi ya ugaidi katika kesi inayomkabili mtu mmoja mzaliwa wa Iran.

Mtu huyo alifikishwa katika mahakama ya mji wa Celle uliyoko kaskazini mwa Ujerumani akituhumiwa kuliunga mkono kundi la kigaidi la al-Qaida kwa kunakili propaganda zake na kuzisambaza kwenye mtandao.

Wanasheria wanasema kuwa kuna wasi wasi mkubwa ya kwamba mtandao wa internet unatumiwa kama mojawapo ya silaha za kigaidi.

Wakati huo huo mahakama ya mjini Stuttgart imemuhukumu kifungo cha miaka miwili na nusu mkurdi kutoka Iraq kwa kosa la kulipelekea fedha kundi la kigaidi la Ansar al Islam la nchini Iraq.