1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Ujerumani yadhamiria kuondosha wanajeshi wake Bosnia.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxp

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amesema kuwa, anataka wanajeshi wa ujerumani waondoshwe taratibu kutoka Bosnia.

Jung amesema, vitendea kazi vya jeshi la Ujerumani vililazimika kuondoshwa mara mbili na kuongeza kuwa hali ya usalama huko Balkan imeimarika.

Kiasi cha wanajeshi 850 wa Ujerumani waliweka maskani yao huko Bosnia pamoja na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Ulaya.

Waziri Jung amesema, serikali ya Ujerumani inafikiria kuliondosha kundi la kwanza la wanajeshi wake kabla ya mwisho wa mwaka huu.