1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Umoja wa Ulaya waahidi msaada kwa Afghanistan

30 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWZ

Umoja wa nchi za Ulaya umetangaza msaada wa takriban Euro milioni 600 kwa Afghanistan katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Kamishna wa mambo ya nje wa umoja wa ulaya Benita Ferrero- Waldner amesema msada huo ni wa kusaidia sekta ya sheria katika vita vyake dhidi ya rushwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier amesema pia kuwepo vikosi vya kijeshi na juhudi za ujenzi wa Afghanistan mpya ni muhimu kwa nchi ya Afghanisatan.

Mkutano wa kimataifa wa siku mbili kuhusu Afghanistan unaendelea mjini Berlin.

Mkutano huo unaangazia maendeleo ya Afghanistan tangu kufanika mkutano kama huo mjini London nchini Uingereza.

Katika mpango wa miaka mitano serikali ya rais Ahmed Karzai wa Afghanistan kwa upande wake imeahidi kuimarisha hali ya usalama, utawala bora

Wakati huo huo tunaarifiwa kwamba mpiganaji wa kujitoa muhanga aliyekuwa ndani ya gari lililokuwa na vifaa vya kulipuka amejivugumiza katika basi lililokuwa limewabeba wanajeshi karika mji wa Herat magharibi mwa Afghaniustan.

Mtu huyo alikufa papo hapo na takriban watu 12 wamejeruhiwa wakiwemo raia.