1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Wanajeshi wa Ujerumani kuendelea na mpango wa "kudumisha uhuru" kwa mwaka mmoja zaidi.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCu7
Rais Vladamir Putin wa Urusi
Rais Vladamir Putin wa UrusiPicha: AP

Bunge la Ujerumani limepiga kura kuviruhusu vikosi vya jeshi la Ujerumani kushiriki kwa mwaka mmoja zaidi katika operesheni inayoongozwa na Marekani dhidi ya ugaidi ijulikanayo kwa jina la kudumisha uhuru.

Muda huo hata hivyo unazungumzia juu ya kupunguzwa idadi jumla ya wanajeshi kutoka 2,008 na kusalia 1,800.

Hivi sasa Ujerumani ina wanajeshi 330 wanaopiga doria katika fukwe za Somalia na Yemen na wanajeshi 100 wa kikosi maalum kinachopambana na ugaidi nchini Afghanistan.

Mtaalamu wa siasa za nje wa chama cha SPD Hans-Ulrich Klose anasema.

“Hakuna asiyekuwa na shaka linapohusika suali la uamuzi wa kijeshi, hata mimi nina shaka shaka, lakini ninaamini kuzuia shughuli za kuendeleza amani kwa wakati huu tulionao usingekuwa uamuzi wa busara“.

Vyama ndugu vya kihafidhina na washirika wao wa chama cha SPD katika serikali inayoongozwa na Kansela Angela Merkel, wakisaidiwa na chama cha upinzani cha Waliberali FDP wameidhinisha mpango huo kwa sauti 436 dhidi ya 101, huku chama cha walinzi wa mazingira na chama cha mrengo wa shoto wakijaribu kuzuia kwa hoja kuwa mpango huo unakwenda kinyume na makubaliano ya Geneva.