1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Waturuki wa Ujerumani wapinga sheria za uhamiaji nchini

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBk5

Makundi ya kituruki hapa nchini Ujerumani yanatishia kususia mkutano wa serikali juu ya kuwajumuisha wageni katika jamii utakaofanyika hapo kesho.

Makundi hayo yanapinga sheria ngumu za uhamiaji hasa juu ya ndoa zinazohusisha raia wakigeni.

Serikali ya kansela Angela Merkel imekataa kubadili sheria hiyo ikisema imeshapitishwa na bunge na itaanza kufanya kazi mara tu itakawekwa saini na rais Horst Köhler.

Sheria hiyo mpya iliyopendekezwa itawahitaji maharusi wapya kutoka nje ya jumuiya ya Ulaya kuwa na umri usio chini ya miaka 18 na waweze kuzungumza kijerumani kabla ya kujiunga na wake au waume zao nchini Ujerumani.

Mwenyekiti wa jumuiya ya waturuki nchini Kenan Kolat amesema sheria hiyo ni kibaguzi.

Vikwazo hivyo vimewekwa ili kusaidia kuzuia kile kinachodaiwa kuwa ndoa za lazima.