1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:waziri Steinmeier kufanya ziara nchini Marekani

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHz

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank Walter Steinmeier leo anaenda Washington ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo juu ya uhusiano baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani.

Katika safari hiyo bwana Steinmeier anaongozana na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya bwana Javier Solana pamoja na kamishna wa Umoja huo Benita Ferrero Waldner.

Ujumbe wa bwana Steinmeier unatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekanai bibi Condoleeza Rice hapo kesho jumatatu ili kutayarisha mkutano wa viongozi wa Marekani na wa Umoja wa Ulaya unaotazamiwa kufanyika tarehe 30 mwezi aprili.