1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bhutto afuta ziara ya Dubai kufuatia hali ya kisiasa Pakistan

1 Novemba 2007

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Pakistan amechukua uamuzi huo kufuatia tetesi Rais Musharraf huenda katangaza hali ya hatari

https://p.dw.com/p/C77L
Benazir Bhutto
Benazir BhuttoPicha: AP

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto amefuta ziara yake ya kwenda Dubai kufuatia ripoti kwamba kuna uwezekano wa rais Pervez Musharraf akatangaza hali ya hatari ikiwa mahakama itatoa uamuzi dhidi ya uhalali wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Mahakama kuu nchini Pakistan inatarajiwa kutoa uamuzi baadae wiki hii juu ya ikiwa uchaguzi war ais uliopita ulifanyika kwa mujibu wa katiba.

Rais Musharraf aliahidi kujiuzulu kama mkuu wa jeshi kufikia katikati ya mwezi Novemba ikiwa angeshinda uchaguzi lakini hajasema atacchukua uamuzi gani endapo mahakama itabatilisha ushindi wake.Hali ya kisiasa katika taifa hilo imekuwa tete katika miezi ya hivi karibuni.Waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto alirejea Pakistan baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minane na saa chache baada ya kuwasili mjini Karachi alikaribishwa na shambulio la bomu lililosababisha mauji ya watu 139 na wengine wengi wakajeruhiwa.