1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bhutto autuhumu utawala wa Musharraf

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfVi

LARKANA:

Kiongozi wa Upinzani nchini Pakistan,Benazir Bhutto aliituhumu hii leo serikali ya rais Pervez Musharraf kushindwa kupambana kabisa na waumini wenye siasa kali katika taifa hili la kiislamu la Pakistan.Tuhuma hizi amezitoa siku chache baada ya mtu aliejitoa mhanga kujiripua msikitini na kuua watu 50.Tuhuma za Bibi bhutto zimetoka huku kampeni kwa uchaguzi wa mwezi ujao ikipambamoto. Bhuto akiwahutubia wafuasi wake kiasi cha 25,000 kwao Larkana,Pakistan,

waziri m kuu huyo wa zamani alisema chama-tawala kinabeba jukumu la kuzidi kwa itikadi kali ya kiislamu nchini Pakistan wakati wa enzi yote ya utawala wake.

Serikali ya Pakistan imetangaza leo kwamba itasonga mbele na vita vyake dhidi ya Al Qaeda na watalibani licha ya hujuma ilioua majuzi si chini ya watu 50 msikitini.