1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bi Kidude wa Zanzibar afariki dunia

Admin.WagnerD17 Aprili 2013

Msanii maarufu visiwani Zanzibar, Afrika mashariki na nje ya bara hilo Baraka Khamisi maarufu kwa jina la Bi Kidude, amefariki dunia.

https://p.dw.com/p/18He4
The famous East African Taarab Singer Bi Kidude, The photo was taken by our stakeholder, Muhidin Issa Michuzi from Dar es Salaam, Tanzania. Zugeliefert durch Sudi Mnette. Copyright: Muhidin Issa Michuzi
Sängerin Bi KidudePicha: Muhidin Issa Michuzi

Taarifa ya kifo chake ilitangazwa na jamaa zake hii leo mjini Unguja . Bi Kidude anasemekana alikuwa na miaka zaidi ya 90 . Habari zinasema Marehemu atazikwa Kitumba huko Unguja hapo kesho. Caro Robi wa DW amezungumza na Bi Maryam Hamdani mtu aliyekuwa na Bi Kidude takriban wakati wote na hasa katika safari za burudani nchi za nje na kwanza anaelezea anavyomkumbuka marehemu. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza kitufe cha kusikilizia masikioni hapo chini.

Mwandishi: Caro Robi
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman