1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden: Majadiliano kuhusu deni la Marekani yamepiga hatua

20 Mei 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amejaribu kuwahakikishia viongozi wa ulimwengu kuwa Washington haitoshindwa kulipa deni lake licha ya kiwingu kinachogubika mazungumzo ya kuongeza ukomo wa serikali yake kukopa.

https://p.dw.com/p/4Rc8h
Rais Joe Biden wa Marekani
Rais Joe Biden wa Marekani Picha: Saul Loeb/AFP

Akizungumza kabla ya kukutana na viongozi wa kundi la mataifa manne linalofahamika kama QUAD pembezoni mwa mkutano wa G7 huko Hiroshima nchini Japan, Biden amesema hakuna sababu ya ulimwengu kuwa na wasiwasi juu ya deni la Marekani.

Amesema anaamini mazungumzo yanayoendelea kati yake na wabunge wa Republican yatazaa matunda, akipigia mfano kuwa duru ya pili na ya tatu ya mazungumzo hayo yamepata mafanikio fulani ya kutia moyo.

Serikali ya Biden inatanga kuongeza uwezo wake wa kukopa kufikia dola Trilioni 31.4 lakini wabunge kutoka chama cha Republican wanapinga mapendekezo hayo kwa hoja kwamba deni la nchi hiyo tayari limefikia kiwango cha kutia wasiwasi.