1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK: Steinmeier anakutana na Bayikev nchini Kyrgyzstan

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwK

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier akikamilisha ziara yake ya nchi za Asia ya Kati,amewasili Kyrgyzstan.Steinmeier amekutana na waziri wa kigeni Alikbek Dzhekshenkulov katika mji mkuu Bishkek.Leo Jumamosi,anatazamia kuonana na rais Kurmanbek Bakiyev na waziri mkuu Felix Kulov.Siku ya Ijumaa maelfu ya wafuasi wa upinzani waliandamana kwa siku ya pili kwa mfululizo,kumshinikiza Bakiyev ajiuzulu.Serikali ya rais Bakiyev inatuhumiwa ulajirushwa.Kwa upande mwingine Bakiyev anawashutumu wapinzani kuwa wanapanga njama ya kuipindua serikali.Waziri wa kigeni wa Ujerumani Steinmeier hapo kabla alizizuru Turkmenistan, Uzbekistan na Kazakhstan.