1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK:Mgomo wa upinzani waingia siku ya nne

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCA2

Takriban wafuasi elfu mbili wa upinzani wanaendelea na mgomo katika mji mkuu wa Bishkek nchini Kyrgyzstan.

Wafuasi hao wa upinzani wanamtaka rais Bakiyev ajiuzulu kutoka madarakani.

Mgomo huo umeingia siku yake ya nne leo.

Taifa hilo la zamani la Sovieti katika Asia ya kati limekumbwa na machafuko tangu vikosi vya upinzani vilipompindua rais wa muda mrefu Askar Akayev mnamo mwezi wa tatu mwaka 2005.

Mgomo huo ulianza tangu siku ya jumatano na waandamanaji wamepiga kambi nje ya makao makuu ya serikali mjini Bishkek wakiapa kuwa hawataondoka mpaka rais Bakiyev atakapo jiuizulu.