1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Blinken ainadi Marekani kama mshirika wa usalama Afrika

24 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameipigia debe nchi hiyo na kuitaja kama mshirika bora wa usalama kwa Afrika badala ya kundi la mamluki wa Urusi, Wagner.

https://p.dw.com/p/4bbgs
Cape Verde | Antony Blinken na Ulisses Correia e Silva
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akisalimiana na Waziri Mkuu wa Cape Verde Ulisses Correia e SilvaPicha: Andrew Caballero-Reynolds/AP Photo/picture alliance

Antony Blinken amelituhumu kundi la Wagner kwa unyonyaji wa mataifa yaliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi au yale yanayoshuhudia mizozo hasa katika ukanda wa Sahel.

Mwanadiplomasia huyo ambaye anaitembelea Nigeria kama sehemu ya ziara yake barani Afrika inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya Washington na bara Afrika, amesema Marekani itaendelea kuisaidia Nigeria na washirika wengine wa kikanda katika juhudi za kuleta utulivu katika eneo la Sahel.

Blinken anafanya ziara katika mataifa manne ya Afrika - Cape Verde, Ivory Coast, Nigeria na Angola - huku akiinadi Marekani kama mshirika muhimu wa usalama kwa Afrika na kudumisha ushawishi wa Washington barani Afrika.