1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobs 2015: Washindi wa shindano la DW

24 Juni 2015
https://p.dw.com/p/1Fmf9
GMF 2015 The Bobs Awards Ceremony
Picha: DW/M. Müller

Washindi hao ni pamoja na Avij Roy, mwanablogi mashuhuri wa kutoka Bangladesh na Bonya Blog aliyekuwa akijishughulisha na mada zinazotenganisha mambo ya kidini na dunia. Yeye na mkewe Rafida Bonya Ahmed walikuwa wakiishi Marekani, walipokwenda likizo mjini Dhakar mwezi february mwaka huu wakahujumiwa- mkewe tu ndie aliyesalimika. "Mume wangu hakupata bahati. Yeye ndie aliyekuwa shabaha ya mashambulio. Wamemuuwa," amesema Rafida Bonya Ahmed.

Wafuasi wa itikadi kali wanatuhumiwakuwa nyuma ya mauwaji hayo. Mkewe lakini anaendelea kublogi. Moyo huo wa kijasiri ndio uliowavutia wataalam wa kimataifa hadi kumtunukia tuzo ya Bobs-mageuzi ya kijamii kwa mwaka 2015.

Mmojawapo wa wataalamu wa kimataifa waliowachagua washindi wa Best of Blogs ni mwanaharakati wa haki za binaadamu, Shahidul Alam. Na alikuwa na haya ya kusema: "Ni jukumu la jamii sasa kuwalinda na kuhakikisha wale waliopoteza maisha yao hawakuyapoteza bure." Kanda ya video iliyopewa jina "Zaytoun-mkimbizi mdogo" kanda ya video inayowazinduwa watu kuhusu ukweli wa hali ya mambo kwa wakimbizi wa kipalastina na Syria. Aliyetengeneza kanda hiyo ya video jina lake halikutajwa ili kuyaanusuru maisha yake.

Na mshindi wa tatu ni pendekezo lililotokea Mexico- Rancho Electronicio linalowaeleza wanablogi kuhusu kinga ya data na upelelezi nchini mwake.

Mbali na tuzo zilizoteuliwa na jopo la wataalam kuna tuzo ya washiriki pa iliyotolewa. Inahusu "sababu elfu moja zinazomfanya mtu aipende lugha ya kijerumani“. Tuzo hiyo wametunukiwa wanablogi wawili wanaoishi Teneriffa nchini Uhispania.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Yusuf Saumu