1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA: Juhudi za kupiga vita madawa ya kulevya zasifiwa

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJ4

Rais Horst Köhler wa Ujerumani ameunga mkono juhudi za serikali ya Colombia kupiga vita madawa ya kulevya na wanamgambo wa mrengo wa kushoto.Lakini amesema,juhudi hizo zitafanikiwa ikiwa serikali vile vile itatia maanani maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wakazi walio masikini. Köhler alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake ya siku nne nchini Colombia.Majadiliano hayo yamehusika na ushirikiano kati ya Colombia na nchi za Umoja wa Ulaya katika sekta ya biashara na kupiga vita biashara ya madawa ya kulevya.