1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolt kutetea taji lake la mita 100

4 Agosti 2012

Mwanariadha Usain Bolt ataanza harakati za kutetea taji lake katika mbio za mita 100, naye Mwogeleaji Michael Phelps akiwa na fursa ya mwisho ya kuongeza idadi yake ya medali katika historia ya Olimpiki.

https://p.dw.com/p/15joy
World champion Yohan Blake, left, crosses the finish line ahead of current world-record holder Usain Bolt, second from right, Nesta Carter, right, and Michael Frater to win the 100m final at the Jamaica's Olympic trials in Kingston, Jamaica, Friday, June 29, 2012. Blake pulled a stunner finishing in 9.75 seconds to upset Bolt by 0.11 seconds. (Foto:Collin Reid/AP/dapd)
Jamaika Yohan Blake Usain BoltPicha: AP

Bolt atashiriki mbio za mchujo leo pamoja na wanariadha Yohan Blake na Asafa Powell wote wa Jamaica, na Mmarekani Tyson Gaye. Katika usiku wa mwisho wa uogeleaji, Phelps atajiunga na wenzake wa kikosi cha Marekani katika fainali ya kitengo cha mita mia moja  kupokezana  mara  nne. Mwogeleaji huyo atalenga kunyakua medali yake ya 22 katika michezo ya Olimpiki.

Katika siku ya kwanza ya riadha bingwa mtetezi Muethiopia Tirunesh Dibaba alinyakua dhahabu katika mbio za mita 10,000 wanawake, wakati  alipotimka kwa kasi baada ya kengele kupigwa na kuwashinda mahasimu wake wawili wa Kenya. Dibaba alimtangulia Sally Kipyego kwa takriban mita 30, huku naye bingwa wa dunia Vivian Cheruyiot akinyakua shaba.

Tirunesh Dibaba anafahamika kutimka kasi katika hatua za mwisho mwisho
Tirunesh Dibaba anafahamika kutimka kasi katika hatua za mwisho mwishoPicha: picture-alliance/ dpa

Baada ya ushindi huo, Dibaba alikuwa na habari mbaya kwa mahasimu wake, wakati alipotangaza kuwa atajitosa katika taaluma ya mbio za marathon mwaka ujao, bila kuwacha mbio zake za uwanjani.

Alisema angetaka kuandikisha ukurasa mpya katika kumbukumbu za Olimpiki. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26 hakutoa maelezo zaidi. Lakini kitisho sasa kipo wakati akifuata nyayo za mwanariadha Muethiopia mwenzake Haile Gebrselassie, ambaye alishinda dhahabu katika mbio za mita 10,000 mnamo mwaka wa 1992 na 1996 mfululizo na kisha akaandikisha rekodi ya ulimwengu katika mbio za marathon. Hata hivyo Gebrselassie hakuwahi kushinda nishani ya dhahabu katika Olimpiki katika mbio hizo za kilomita 42.195, jambo ambalo Dibaba amejitolea kutimiza mjini Rio de Janeiro mnamo mwaka wa 2016.

Ijumaa usiku Dibaba alirejea katuika jukwaa kubwa miaka minne baada ya kunyakua dhahabu mbili katika mashindano ya Olimpiki Beijing mnamo mwaka wa 2008, katika mbio za mita 5,000 na 10,000, na kukosa kushiriki mashindano mawili ya ubingwa wa ulimwengu kutokana na matatizo ya majeraha mwaka jana.

Watazamaji na muhimu zaidi mahasimu wake wa Kenya walishindw akumfuata wakati Dibaba alipotimka kama desturi yake zikiwa zimesalia mita 500 kumaliza na akanyakua ushindi katika muda bora mwaka wa 2012 wa dakika 30. 20.75. Sally Kipyego alikuwa wa pili na 30.36.37 na mkenya mwenzake Vivia Cheruyiot ambaye alishinda mara mbili katika kitengo hicho wakati Dibaba alikuwa nje, katika mwaka wa 2011, akachukua shaba katika muda wa 30.30.44, ukiwa ni muda wake bora na wakaipa Kenya medali za kwanza katika michezo ya London.

Uhasimu kati ya Ethiopia na Kenya katika masafa marefu ni wa jadi
Uhasimu kati ya Ethiopia na Kenya katika masafa marefu ni wa jadiPicha: dapd

Kipyego na Cheruyiot walionekana ni kama wapiti njai tu kutokana na kasi ya Dibaba na hawakutoa ushindani wowote katika sekunde za mwisho hata ingawa walifahamu mtindo maarufu wa Dibaba naye Dibaba akajaribu bahati yake mbele kwa kuongeza kasi.

Kipyego alisema alisema alijaribu kuongeza kasi na kumfanya kila mtu kuchoka, lakini kwa bahati mbaya hilo halikutendeka na Dibaba. Hivyo ina maana kuwa katika awamu ya kwanza ya uhasimu wa kenya na Ethiopia, ambao ni wa amsafa marefu sawa na ule wa Marekani na Jamaica katika masafa mafupi, iliwaendea Waethiopia.

Wote watakutana tena Jumanne katika mbo za mchujo wa mita 5,000 na wameapa kuwa tayari wka awamu ya pili. Wanariadha wa kike nchini kenya wameanza kufanya vyema zaidi baada katika ulingo ambao ulitawaliwa na wanariadha wa kiume waliokuwa wakinyakua medali. Cheruyiot alisema baada yam bio za jana kuwa , miaka minne au mitano iliyopita hawakuwa wanajiamini, lakini sasa kila mtu anakimbia.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA

Mhariri: Sekione Kitojo