1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomu lamshtusha Ban Ki Moon mjini Baghdad

Maja Dreyer22 Machi 2007

Mita 50 tu kutoka jengo ambamo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki, walikuwa wakijibu masuala ya waandishi wa habari, bomu lilpiga katika eneo hilo kati kati ya mji wa Baghdad. Ban Ki Moon anaitembelea Iraq kwa mara ya kwanza kuzungumzia mpango wa miaka mitano wa kujenga upya Iraq.

https://p.dw.com/p/CHHj
Ban Ki Moon kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad
Ban Ki Moon kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini BaghdadPicha: AP Graphics

Ni sauti mlio wa roketi ilisikika nje tu ya jengo ambapo kulifanyika mkutano na waandishi wa habari. Jukwaani, katibu mkuu Ban Ki Moon alishtushwa na kuingiwa na hofu huku akiangalia kushoto na kulia. Alipoona lakini hakuna mlipuko mwingine aliendelea kama kawaida. Hakuzungumzia shambulio hili hata kidogo, lakini baada ya kujibu swali moja jingine, Ban Ki Moon na waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki waliondoka.

Hivyo, katibu mkuu huyu, akiwa katika ziara hii yake ya kwanza nchini Iraq tangu kuingia maradakani amejiona mwenyewe vile hali ya usalama ilivyo katika nchi hiyo. Kabla ya hapo Ban Ki Moon alielezea malengo yake aliyoyazungumzia katika mkutano wake na waziri mkuu wa Iraq al-Maliki. Alisema mazungumzo haya yalituwama: “juu ya masuala kadhaa yakiwemo hali ilivyo hivi sana, na namna Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa inaweza kuwasaida watu wa Iraq kurudisha amani na usalama, ustawi, uhuru na demokrasia.”

Mazungumzo kati ya Ban Ki Moon na waziri mkuu al-Maliki yanahusu pia mpango wa miaka mitano wa kuijenga upya Iraq ulioweka masharti ambayo Iraq inatarajiwa kuyakamilisha katika muda huo. Ban aliiomba jumuiya ya kimataifa iisaidie Iraq katika kutekeleza mpango huo.

Ziara ya Ban Ki Moon ambayo haijatangazwa hapo awali inafanyika wakati kuna habari nyingine za vurugu nchini Iraq. Wanajeshi wengine watatu wa Marekani wanaripotiwa kuuawa katika mapigano mjini Basra. Wakati huo huo jeshi la Marekani limetangaza kuwa limewakamata viongozi wa mtandao wa Shiit ambal unaaminika kupanga shambulio kubwa dhidi ya jeshi hilo mwanzoni mwa mwaka huu.

Maafisa wa serikali ya Marekani wamesisitiza kuwa lazima sasa suluhisho la kisiasa litafutwe. Mwenye matumaini katika suala hilo ni mkuu wa mambo ya kimataifa katika wizara ya mdahalo wa kitaifa ya Iraq, Bw. Saad Yousif al-Muttalibi. Naye alisema: “Mengi ya makundi hayo sasa yanatafakari kuwa yatafaulu zaidi kwa kujihushisha na mdahalo na wala siyo kurusha mawe au mabomu dhidi ya watu.”

Al-Muttalabi aliongeza kusema kuwa serikali yake tayari imeanza mazungumzo na makundi kadhaa, lakini hadi sasa mazungumzo haya hayajafanikiwa kwa sababu makundi hayo yanadai jeshi la Marekani liondoke moja kwa moja.