1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bonn. Mgomo wazidi kukua.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC24

Sekta ya huduma ya chama cha wafanyakazi cha Ver.di kimepanua hatua yake ya mgomo katika shirika la simu la Ujerumani Deutsche Telekom , ambalo lilikuwa linahodhi huduma za simu nchini.

Chama hicho cha wafanyakazi kimewataka wanachama wake katika kampuni hilo wapatao 14,000 nchini Ujerumani kutofanya kazi.

Mgomo huo unafanyika kupinga mpango wa kampuni hilo wa kufanya mageuzi.

Telekom inataka kuhamisha nafasi 50,000 za kazi kwenda katika huduma mpya kwa wateja zilizoanzishwa ambako wafanyakazi watafanyakazi kwa muda mrefu kwa malipo kidogo.