1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borrell: Mapigano yasitishwe kuruhusu misaada kuingia Gaza

Lilian Mtono
23 Oktoba 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameunga mkono miito ya kusitishwa mapigano kati ya Isreal na Hamas ili kuruhusu ufikishwaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4Xu0T
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.Picha: FREDERICK FLORIN/AFP

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameunga mkono miito ya kusitishwa mapigano kati ya Isreal na Hamas ili kuruhusu ufikishwaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza.

Amewaambia waandishi wa habari huko Luxembourg kwamba suala la msingi kwa sasa ni kufikishwa kwa misaada ya kiutukwenye eneo hilo, na kukumbushia mchakato wa amani ambao amesema umesahaulika kwa muda mrefu.

Soma pia:Israel yaendeleza mashambulizi Gaza

Borrell yuko Luxembourg kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, wanaokutana kujadili mzozo wa Mashariki ya Kati na kuendelea kuisaidia Ukraine.

Jana Jumapili, Rais Joe Biden wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walizungumza tena kwa simu na kukubaliana misaada kuendelea kupelekwa Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Rafah.