1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brahimi akutana na Assad,aionya dunia

16 Septemba 2012

Mjumbe wa kimataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi ameonya baada ya kukutana na rais Bashar al-Assad Jumamosi(15.09.2012) kuwa mzozo unaozidi kukua nchini Syria unatishia eneo lote la mashariki ya kati pamoja na dunia.

https://p.dw.com/p/169r7
++++ Alternativer Ausschnitt +++ epa03398423 A handout photo made available by Syria's Arab News Agency SANA shows Syrian President Bashar Assad (C-R) meeting with the U.N.-Arab League envoy, Lakhdar Brahimi (C-L), in Damascus, Syria on 15 September 2012 for talks that focused on the 18-month-old crisis in the country. Brahimi_s meeting with Assad is the first since he has replaced the former UN Secretary General Kofi Annan. Brahimi, who is on a three-day visit to Syria, held a series of meetings in Damascus with Syrian officials and opposition leaders in order to shape a clear perspective for his future initiative to end the crisis. EPA/SANA / HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mkutano kati ya rais Bashar Assad na mjumbe wa kimataifa Lakhdar BrahimiPicha: picture-alliance/dpa

Urusi , ambayo  ni  mshirika  mkubwa  wa  Syria, imesisitiza  kuwa " haing'ang'anii " kiongozi  fulani  nchini  Syria,  lakini  imeonya  kuwa itazuwia  azimio  lolote  jipya la  baraza  la  usalama  la  umoja  wa mataifa  lenye  lengo  la  kumshinikiza Assad, mshirika  wa  muda mrefu  wa  Urusi.

"Mzozo  huu ni  hatari  na  unazidi  kuwa  mbaya , na  ni  kitisho  kwa watu  wa  Syria , eneo  zima  la  mashariki  ya  kati na  dunia, amesema  Brahimi  aliyeteuliwa   hivi  karibuni , na  kuchukua  nafasi kama  mjumbe  mpya  mapema  mwezi  huu  nafasi  iliyoachwa  wazi na  katibu  mkuu  wa  zamani  wa  umoja  wa  mataifa  Kofi  Annan.

Syria's Deputy Foreign Minister Faisal Mekdad (R) welcomes United Nations (U.N.)-Arab League peace envoy for Syria Lakhdar Brahimi (L) upon his arrival at a hotel in Damascus September 13, 2012. Brahimi arrived in Syria on Thursday, his first trip to the country since taking up his post, pledging to work to end violence in which more than 27,000 people have been killed. REUTERS/Khaled al-Hariri (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Mjumbe wa kimataifa Lakhdar Brahimi alipowasili mjini DamaskusPicha: Reuters

Assad ataka majadiliano

Assad , akinukuliwa  na  televisheni  ya  taifa , amesema  majadiliano baina  ya  Wasyria  ni  muhimu  kuweza  kuleta  suluhisho  na  kutoa wito  kwa  mataifa  ya  kigeni  kuacha  kuwapatia  silaha  mahasimu wake.

"Tatizo  kubwa  nchini  Syria  ni  lile  ya  kuchanganya  siasa  na  kazi inayofanyika kwa  mapambano," amesema. Kazi  ya   kisiasa inaendelea , hususan  kwa  kutoa  wito  wa  kufanyika  majadiliano kati  ya  Wasyria  yaliyo  katika  misingi  ya  matakwa  ya  Wasyria.

"Mafanikio  ya  hatua  hii  ya  kisiasa  inategemea  utoaji  wa  mbinyo kwa  nchi  ambazo  zinafadhili  na  kuwapa  mafunzo  magaidi, na ambazo  zinaingiza  silaha  nchini  Syria, hadi  pale  zitakapositisha hatua  hiyo", amesema  Assad. Miezi  18  tangu  kuanza  kwa  mzozo huo  ambao  umekuwa  hatari  na  ambao  hauonekani  kufikia mwisho, Assad  amesema  serikali  yake  itatoa  ushirikiano  kwa juhudi  za  kweli  za  kuutatua  mzozo  huo, iwapo juhudi  hizo haziegemei  upande  mmoja  na  ni  huru.

The Joint Special Envoy for Syria, Kofi Annan poses in his office before a meeting with Major-General Robert Mood of Norway at the United Nations in Geneva July 20, 2012. REUTERS/Denis Balibouse (SWITZERLAND - Tags: POLITICS MILITARY)
Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi AnnanPicha: Reuters

Brahimi, mwenye  umri  wa  miaka  78, mtu  ambaye  ni mkongwe katika  masuala  ya  utatuzi  wa  mizozo,  raia  wa  Algeria, pia amekutana  na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Syria  Walid Moallem  na viongozi  wa  upande  wa  upinzani  ambao unavumiliwa  rasmi  na  serikali  ya  Syria   tangu  alipowasili  mjini Damascus  siku  ya  Alhamis.

Suluhisho litatoka  kwa  Wasyria wenyewe

"Kuna  haja  ya  pande  zote  kuunganisha  juhudi  zao  ili  kutafuta suluhisho  la  mzozo  huu, kutokana  na  umuhimu  wa  Syria  katika eneo  hili,  na  ushawishi  wa  mzozo  huu  katika  eneo  lote" , Amesema  Brahimi.

"Suluhisho  pekee  linaweza  kupatikana  kutoka  kwa  Wasyria wenyewe".

Amesema  kwa  sasa , "hana  mpango", kuweza  kupambana  na mzozo  huu, lakini  mkakati  utaundwa baada  ya  kusikiliza  pande zote  za  ndani, kimkoa  na  kimataifa.

Brahimi  ameonya  alipowasili  kuwa  mzozo  huo , unaendelea  kuwa mbaya. Yuko  katika  ziara  yake  ya  kwanza  mjini  Damascus tangu  alipochukua  nafasi  ya  Annan , ambaye  amejitoa  baada makubaliano  ya  amani  ambayo  amekuwa  mpatanishi  kushindwa.

Brahimi  siku  ya  Ijumaa(14.09.2012)  alikutana  na  viongozi  wa  makundi  ya upinzani  nchini  Syria  ambao  wamesema  wanaleta  mawazo mapya ,  katika  juhudi  za  kuleta  amani . Alikutana  na  makundi  ya upinzani ambayo  yanavumiliwa  na  utawala  wa  Assad  kama  vile National  Coordination Committee ,  kamati  ya uratibu  wa  taifa kwa  ajili  ya  mabadiliko  ya  kidemokrasia, ambayo  inajumuisha makundi  ya Waarabu  wazalendo, Wakurdi  na  wasoshalisti.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Idd Ssessanga