1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRASILIA : Köhler na Silva wahimiza biashara huru

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL3

Rais Horst Köhler wa Ujerumani na rais mwenzake wa Brazil Luiz Inacio da Silva wametowa wito wa kuwepo kwa usawa zaidi duniani.

Wakizungumza na waandishi wa habari viongozi hao wote wawili wamesema kukamilishwa kwa mafanikio mazungumzo ya biashara ya Duru ya Doha ni muhimu katika kupambana na umaskini.Rais wa Brazil ameutaka Umoja wa Ulaya kufunguwa masoko yake ya kilimo na kupunguza ruzuku yake kwa kilimo.

Köhler yuko katika ziara ya siku 12 Amerika ya Kusini ambayo tayari imemfikisha Paraguay na ambayo pia itamfikisha Colombo.