1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRASILIA : Rais Lula ashinda uchaguzi Brazil

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxu

Mamlaka ya uchaguzi nchini Brazil imethibitisha kwamba Rais Luiz Inacio da Siilva Lula ameshinda kipindi kengine madarakani katika marudio ya uchaguzi hapo jana.

Maafisa wa uchaguzi wanasema uchaguzi umefanyika kwa utulivu ambapo Lula amejipatia ushindi wa zaidi ya asilimia 60 ya kura kumshinda mpinzani wake Geraldo Alckmin.

Wakati uchaguzi huo ulipokuwa ukiendelea kufanyika Rais huyo anayetetea wadhifa wake ametangaza nia yake ya kuwa na mazungumzo na wapinzani wake wa kisiasa ili kuboresha mazingira ya kuongoza nchi hiyo kwa kipindi chake cha pili madarakani.

Lula amesisitiza kwamba anataka kuunda muungano unaohitajika kutekeleza miradi yote mikubwa ambayo anaamini inahitajiwa na Brazil.