1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Braunschweig wawabwaga Hanover

7 Aprili 2014

Wakati msimu ukielekea ukingoni klabu inayoshika mkia Eintracht Braunschweig ilijaribu kuyaweka hai matumaini ya kusalia katika ligi kuu ya Bundesliga baada ya kuwacharaza Hanover magoli matatu kwa bila

https://p.dw.com/p/1BdMh
Fußball Bundesliga 29. Spieltag Eintracht Braunschweig - Hannover 96
Picha: picture-alliance/dpa

Hii ina maana ni pointi nne tu zinazozitenganisha timu sita za mwisho. Mchezaji mzaliwa wa Kongo Domi Kumbela aliwapa Braunschweig uongozi kabla ya mshambuliaji Mnorway Havard Nielsen kufanya mambo kwua sifuri kwa bila. Hanover kisha wakapata pigo baada ya kiungo Andre Hoffman kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 62 kwa kucheza rafu. Katika mechi nyingine ya jana Hoffenheim iliikaba Hertha Berlin kwa sare ya goli moja kwa moja. Andreas Beck ni mchezaji wa Hoffenheim

Siku ya Jumamosi, mabingwa Bayern, walipata kichapo cha kwanza tangu Oktoba mwaka wa 2012 baada ya rekodi yao ya mechei 53 bila kushindwa kufikia kikomo mikononi mwa Augsburg waliowafunga goli moja kwa sifuri. Kocha Pep Guardiola alicheza karata kwa kukichagua kikosi dhaifu huku akiutupia jicho moja mchuano wa Jumatano dhidi ya Manchester United katika Champions League.

Borussia Dortmund wanaendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili ya msimamo wa Bundesliga
Borussia Dortmund wanaendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili ya msimamo wa BundesligaPicha: picture-alliance/dpa

Nambari mbili Borussia Dortmund walijipa morale kutokana na ushindi wa magoli mawili kwa moja nyumbani dhidi ya Wolfsburg kabla ya mechi yao ya kesho ya champions league dhidi ya Real Madrid.

Schalke sasa wako katika nafasi ya tatu nyuma ya Dortmund na pengo la points tatu, baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya goli moja kwa moja na Werder Bremen.

Katika upande wa chini, Stuttgart waliimarisha nafasi zao za kuepuka shoka la kushushwa ngazi kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Freiburg. Nuremberg imeanguka katika nafasi ya pili kutoka nyuma baada ya kuonjeshwa mabao mawili kwa sifuri na Borussia Moenchengladbach, ambao walisonga hadi nafasi ya nne na katika nafasi ya kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa kutokana na uzembe wa Bayer Leverkusen.

Leverkusen walimtimua kocha wao Sami Hyppia baada ya kuduwazwa magoli mawili kwa moja na washika mkia Hamburg na kuwaweka katika hli ngumu y akujikatia tikiti ya kucheza katika Champions League

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman