1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil kufuta madeni yake kwa nchi 12 za Afrika

Admin.WagnerD28 Mei 2013

Hatua ya serikali ya Brazil ya kufuta au kurekebisha madeni yake yenye thamani ya Dola milioni 900 kwa nchi 12 za Afrika,ni ishara ziada ya mikakati ya kuimarisha masilahi yake katika eneo linalonawiri kiuchumi.

https://p.dw.com/p/18fqJ
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff
Rais wa Brazil, Dilma RousseffPicha: REUTERS

Hatua hiyo imetolewa na Rais wa Brazili Dilma Rouseff mjini Addis Ababa wakati alipohudhuria sherehe za miaka 50 ya umoja wa Afrika,safari yake ya tatu ndani ya miezi mitatu barani Afrika ambapo Brazili imekuwa na ukaribu wa kitamaduni na mshikamano wa kiuchumi na bara hilo.

Rousseff amesema hatua hiyo ya kufuta madeni kwa nchi za Afrika,ni sehemu ya juhudi za Brazili kuiinua uchumi wa Afrika,ambayo inainukia kiuchumi haraka ulimwenguni.

Tanzania na  Congo Brazzaville zimepumua

Miongoni mwa nchi 12 ambazo zimefutiwa madeni na Brazili ni pamoja na Congo Brazzaville ambayo ilikuwa na madeni makubwa yenye thamani ya Dola milioni 352,ikifuatiwa na Tanzania ambayo inadaiwa  Dola milioni 237.

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho KikwetePicha: AP Photo

Mbali na hatua hiyo ya kufuta madeni kwa nchi hizo,Rais Rousseff  amesema serikali yake ina mpango wa kusaidia sekta za viwanda kwa nchi za Afrika lakini na Amerka ya kusini,nchi ambazo zinaongoza kwa wakaazi weusi baada ya Nigeria, ambazo sasa zina uhusiano wa kitamaduni na kihistoria na nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kireno kama Angola,Msumbiji,Guinea-Bissau , Sao Tome na Principe na Cape Vade.

Amesema Amerika ya Kusini ambayo ina watu milioni 200,kwa sasa  ni  mwanachama wa umoja wa nchi zinazoinukia kiuchumi duniani BRICS ambazo ni Brazili,Urusi,India,China na Afrika Kusini.

Aidha Rais huyo wa Brazil ameongeza kwamba  kutokana napato la ndani dola trilioni 2.425 iliopata Brazili kwa mwaka,2012 nchi hiyo kwa sasa imechukua nafasi ya saba duniani kiuchumi,kwa ukuaji wa asilimia 3.5 mwaka huu 2013.

 Mkakati wa kuipiga jeki  Afrika kiuchumi.

b Rais huyo wa Brazili anaendeleza siasa iliowekwa na aliekuwa Rais wa nchi hiyo Luis Inacio Lula da Silva ambaye aliiweka Afrika katika kipaombele cha sera za nje za Brazili.

Rais wa Nigeria, Jonathan Goodluck
Rais wa Nigeria, Jonathan GoodluckPicha: AP

Kwa upande wake profesa  mambo ya kimataifa katika taasisi ya Getulio Vargas  amelimbia shirika la habari la AFP, Brazili inatilia maanani Afrika mabayo inainukia kwa kasi kiuchumi duniani,ambayo hapo awali ilikuwa nyuma katika maendeleo ya kuchumi.

Amesema hatua hiyo si tu inainua uchumi,bali mahusiano ya kisiasa na nchi 54 za Afrika ambazo ni wanachama wa Umoja wa mataifa ambao Brazili inazitumia kuomba nafasi katika baraza la usalama  la umoja huo,baada nchi hizo hivi karibuni kusaidia Brazili kuchaguliwa kuliongoza shirika la biashara la kimataifa, WTO.

Biashara ya brazili barani Afrika iliongezeka kutoka dola bilioni 5 mwaka 2002 na kufikia dola 26.5 bilioni mwaka 2012 ambapo kwa sasa ina balozi zake 37 katika bara la Afrika.

Brazili pia imewekeza  mamilioni ya Dola katika sekta ya mafuta,gasi na nisheti mbadala nchini Nigeria.

Ingawa uwepo wa Brazili barani Afrika,ni mdogo ukilinganisha na China,lakini miradi yake inakwenda sambamba na maendeleo ya kiuchumi ya nchi za Afrika,hasa msaada wake katika sekta ya kilimo,chakula,uzalishaji mafuta na  miradi ya kijamii yenye malengo ya kuondoa umasikini katika nchi hizo.

Mwandishi:Hashim Gulana/AFP

Mhariri: Abdul-Rahman