1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRAZILIA: Rais wa Ujerumani ziarani Amerika ya Kusini

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLM

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amewasili katika mji mkuu wa Brazil,Brazilia.Hicho ni kituo cha pili cha ziara yake ya siku 12 katika bara la Amerika ya Kusini.Leo atakutana na rais mwenzake Luiz Inacio Lula da Silva.Baadae ataelekea Sao Paulo,mji unaojulikana kama ni ngome ya uchumi wa Brazil.Huko Köhler atakutana na wamiliki makampuni.Majadiliano yake na matajiri hao yatahusika na dhima za kijamii za makampuni.Rais Köhler aliyeanza ziara yake nchini Paraguay, anatazamia kwenda Colombia.