1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BREMEN: Msaada kutolewa tena kwa Wapalestina

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDl

Umoja wa Ulaya unataka tena kushirikiana moja kwa moja na serikali ya Wapalestina ya umoja wa kitaifa,lakini ni pamoja na wanachama wasiohusika na Hamas kinachofuata siasa kali.Uamuzi huo umepitishwa na mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya kwenye mkutano wao usio rasmi.Vile vile taasisi za Kipalestina zitasaidiwa tena kifedha.Misaada ya kiutu ya Umoja wa Ulaya ilipunguzwa baada ya chama cha Hamas kuunda serikali yake mwaka mmoja uliopita.Mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wao mjini Bremen,kaskazini mwa Ujerumani, vile vile wamesema,wanaamini kuwa sasa utaratibu wa amani wa Mashariki ya Kati una nafasi nzuri ya kufanikiwa.