1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BREMEN:Pana fursa ya kuleta amani katika mashariki ya kati asema Solana

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDb

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya bwana Javier Solana amesema, kuwa pana fursa ya kuleta amani katika mashariki ya kati.

Bwana Solana amesema hayo baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya uliofanyika katika mjni wa Bremen kaskazini mwa Ujerumani.

Mawaziri hao pia wameunga mkono mpango wa amani uliofufuliwa kwenye mkutano wa nchi za Umoja wa kiarabu uliofanyika mjini Riyadh .

Hatahivyo mawaziri wa Umoja wa Ulaya wamesema kuwa watashirikiana na serikali ya Palestina, lakini bila ya kuwasiliana na wajumbe wa chama cha Hamas waliomo katika serikali hiyo.

Nchi za Umoja wa Ulaya ziliisusia serikali ya Palestina iliyokuwa inaongozwa na Hamas kutokana na serikali hiyo kukataa kuitambua Israel.